• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkakati kupunguza uagizaji wa mafuta ya kula waibuliwa

    (GMT+08:00) 2019-06-27 18:49:13

    Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari) imeanza mkakati wa kupunguza uagizaji wa mafuta ya kula kutoka nje ya nchi baada ya kuanza kuzalisha mbegu za alizeti zilizothibitishwa ubora kwa ajili ya kutumiwa na wakulima na hatimaye kuzalishwa kwa wingi.

    Kupitia mkakati huo tayari Kituo cha Utafiti wa Kilimio Ilonga, Kilosa mkoani Morogoro, kimepewa jukumu la kuzalisha mbegu hizo za alizeti ikiwamo ya rekodi ambayo imeanza kutumika kwa wakulima.

    Mwaka huu pekee Tari imeazalisha mbegu ya alizeti aina ya Rekodi tani 37.8 ambazo zimeshasambazwa kwa wakulima.

    Tari imesema Ekari 18,500 zitapandwa na wakulima katika mikoa mbalimbali ya uzalishaji wa alizeti ikiwamo Singida, Dodoma na Morogoro ambayo imewekewa mkakati wa kulima zao hilo.

    Tari pia inapanga kutoa utafiti mwingine wa mbegu ya alizeti itakayokuwa na ubora kuliko mbegu yoyote iliyoko sokoni kwa sasa ili kuongeza uzalishaji wa mafuta maradufu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako