• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • DODOMA YAKARIBISHA WAWEKEZAJI VIWANDA, MASOKO

    (GMT+08:00) 2019-06-28 18:45:11

    Mkoa wa Dodoma umealika wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kutumia uwepo wa fursa lukuki za uwekezaji kuwekeza katika sekta za ujenzi wa viwanda, miundombinu, masoko, kuchakata na kuongeza thamani mazao.

    Akitangaza fursa hizo kwenye kongamano la siku mbili la uwekezaji mkoani humo, Katibu Tawala wa Mkoa, Maduka Kessy amesema mkoa umefungua milango kwa wawekezaji wa ndani na nje kuchangamkia fursa nyingi zilizomo katika mkoani huo.

    Kessy amezitaja fursa hizo kuwa ni za kilimo cha maembe, alizeti na mazao ya misitu, ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji, mizinga nyuki ya kisasa na ufugaji na uvuvi.

    Pia ujenzi wa viwanda mbalimbali hasa vya vifungashio, vya maziwa, ngozi na vyakula vya mifugo.

    Alitaja fursa nyingine kuwa ni ujenzi wa miundombinu ya masoko, uwekezaji katika ujenzi wa maghala, vituo vya mabasi, mji wa kibiashara na maegesho ya magari ya mizigo.

    Amesema kutokana na jiografia ya nchi inapakana na nchi sita za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia na Msumbiji, hivyo ni rahisi wawekezaji kuzitumia nchi hizo kama masoko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako