• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Michael Joseph ateuliwa kaimu afisa mtendaji mkuu wa Safaricom

    (GMT+08:00) 2019-07-02 19:54:39

    Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imemteua Michael Joseph kuwa kaimu afisa mtendaji mkuu wake, baada ya kufariki kwa aliyekuwa mkuu wake Bob Collymore.

    Michael Joseph aliwahi kuwa mkurungezi wa kampuni hiyo na hadi uteuzi wake alikuwa mwenyekiti wa bodi ya shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways.

    Bob Collymore aliisaidia kampuni hiyo kukua na kuongeza wateja wake kutoka 15, 000 tu miaka 2000 hadi milioni 15.

    Aidha faida ya safaricom iliongezeka chini ya uongozi wake na kufikia shilingi bilioni 251 kipindi cha fedha kilichokamilika Machi 2019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako