Pakistan, ambayo ni mnunuzi mkubwa wa chai ya Kenya imekuwa na mdororo wa sarafu yake kwa asilimia 20 ndani ya mwaka mmoja uliopita hku nao mfumko wa bei ukifikia asilimia 9.
Baraza la kiuchumi la kitaifa nchini Pakistan limesema uchumi unatarajiwa kupungua hadi asilimia 2.4 na mfumko wa bei kupanda hadi asilimia 13.
Mwenyekiti wa chama cha wauza chai wa Afrika Mashariki Peter Kimanga amesema mauzo ya chai kwenda Sudan na Iran piayamepungua kufuatia misukosuko ya kisisasa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |