• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: NDC kukopesha wakulima matrekta

    (GMT+08:00) 2019-07-02 19:55:51
    Mkurugenzi mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) nchini Tanzania, Profesa Damian Gabagambi amesema katika msimu wa maonyesho ya 43 ya sabasaba wameandaa mkakati maalumu wa kuwakopesha wakulima wa vijijini matrekta kwa kutumia barua.

    Amesema barua hiyo ya maombi inapaswa kutoka kwa ofisa mtendaji wa kata kupitia kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji na Mkurugenzi wa halmashauri anayotoka.

    Amesema hatua hiyo imefikiwa ili kupunguza matumizi ya jembe la mkono na kuendana na kasi ya uchumi wa viwanda kwa kumgusa mkulima mmojammoja.

    Maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa yalianza rasmi Juni 28, 2019 na yanatarajiwa kukamilika Julai 13, 2019 huku yakishirikisha zaidi ya nchi 35.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako