Umoja wa Mataifa umechukua tahadhari kubwa kuhusu hali ya kibinadamu baada ya mamia ya watu kuuawa na kujeruhiwa katika vitendo vya kimabavu vilivyotokea katika maeneo ya kaskazini magharibi mwa Syria. Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amewaambia waandishi wa habari kuwa mashambulizi dhidi ya miundombinu ya kiraia na ongezeko la idadi ya watu wanaokimbia makazi yao linashuhudiwa na maeneo yanayodhibitiwa na yale yasiyodhibitiwa na serikali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |