• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 13 baraza la Davos la majira ya joto wafungwa

    (GMT+08:00) 2019-07-03 19:35:58
    Mkutano wa 13 wa baraza la Davos la majira ya joto umemaliza ajenda zote na kufungwa huko Dalian, China. Mkutano huo uliokuwa na kaulimbiu ya "Nguvu ya Uongozi 4.0: Njia ya Mafanikio ya Utandawazi katika Zama Mpya" umefanya shughuli zaidi ya 200 ikiwemo mazungumzo kati ya wafanyabiashara, matamasha ya utamaduni na makongamano maalumu. Viongozi wa sekta za siasa na biashara, wataalamu, wasomi na wajumbe wa vyombo vya habari zaidi ya 2000 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 90 kote duniani wamehudhuria mkutano huo, na kujadili ajenda motomoto ikiwemo mtandao wa 5G, utandawazi, akili bandia, mabadiliko ya hali ya hewa na magari yasiyo na madereva.

    Mustakabali wa uchumi wa China, sera mpya za China kwa makampuni ya kigeni, mabadiliko ya mtindo wa mitaji ya China zimeendelea kuwa mada kuu zilizojadiliwa kwenye mkutano huo. Ishara za kuzidi kufungua mlango na kushikilia mageuzi zinazotolewa na China zimepongezwa na pande mbalimbali, wageni wengi wanaoshiriki kwenye mkutano huo wana imani na matarajio kuhusu nguvu ya China na mipango ya China katika kuhimiza maendeleo ya uchumi wa dunia.

    Siku hiyo waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang pia amefanya mazungumzo na wajumbe 200 wa sekta za viwanda na biashara, fedha, jumuiya ya washauri mabingwa, na vyombo vya habari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako