• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Venezuela atarajia kufikia makubaliano na kundi la upinzani

    (GMT+08:00) 2019-07-03 19:36:14

    Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amesema huko Caracas kuwa serikali ya nchi hiyo inatilia maanani kufanya mazungumzo na upinzani, huku akizitaka pande mbili kufikia makubaliano yenye maelewano, amani, mazungumzo na demokrasia ndani ya mwaka huu chini ya uungaji mkono wa wananchi.

    Rais Maduro ametoa hotuba ikulu akisema serikali ya nchi hiyo inaunga mkono kujenga mfumo wa kawaida wa mazungumzo na utatuzi wa mgogoro, ili kufungua mlango wa mazungumzo kwa pande mbalimbali za upinzani. Anaona watu wote wa Venezuela wanatakiwa kufanya juhudi kulifanya taifa liwe zuri zaidi na kuirejesha nchi hiyo katika hali ya kawaida.

    Pia amelaani vitendo vya kuharibu mchakato wa mazungumzo, na kusema suala la nchi hiyo linatakiwa kutatuliwa na wananchi, na nguvu za nje haziwezi kuingilia kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako