• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 40 wauawa katika shambulizi la anga dhidi ya kituo cha wahamiaji cha Libya

    (GMT+08:00) 2019-07-03 19:37:07

    Shambulizi la anga limefanywa dhidi ya kituo cha wahamiaji kilichopo katika kitongoji cha Tripoli, mji mkuu wa Libya na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.

    Msemaji wa wizara ya afya ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa Bw. Malek Mersek amesema, hadi sasa watu 40 wameuawa na wengine zaidi ya 80 wamejeruhiwa katika shambulizi hilo dhidi ya kituo cha kizuizini kilichoko maskani ya Tajoura ya Tripoli.

    Hadi sasa mambo mengine kuhusu shambulizi hilo bado hayajafahamika. Muda mfupi baada ya shambulizi hilo, serikali ya nchi hiyo imetoa taarifa ikiilaumu Jeshi la LNA linaloongozwa na Jenerali Khalifa Hafta kuhusika na shambulizi hilo.

    Habari nyingine zinasema shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeeleza wasiwasi wake kuhusu mashambulizi ya anga karibu na kituo cha kizuizini cha wahamiaji huko Tripoli. Shirika hilo limesema, raia kwamwe hawawezi kuwa shabaha ya shambulizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako