• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Mauzo ya nje ya Uganda ya bidhaa kama vile dhahabu na kahawa yapungua

    (GMT+08:00) 2019-07-03 19:48:17
    Mauzo ya nje ya Uganda ya bidhaa kama vile dhahabu, kahawa yamepungua mwezi Aprili kutokana na kushuka kwa uzalishaji.

    Ripoti ya utendaji wa uchumi inayotolewa kila mwezi na wizara ya fedha inasema mauzo ya vanilla, Sukari na mahindi ndio yameongezeka.

    Ripoti hiyo inaonyesha kuwa mauzo ya nje ya dhahabu yalishuka kwa tani 2.2 kutoka tani 8.6 za mwezi Machi.

    Mwaka 2018 hata hivyo dhahabu iliiletea Uganda dola 549 ikilinganishwa na dola milioni 339 za mwaka 2017.

    Mauzo ya jumla ya Uganda kwenye soko la jumuiya ya Afrika Mashariki yalipungua kwa asilimia 9.8 katika kipindi kilichokamilika Aprili 2019.

    Kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki, Kenya inasalia kuwa mshirika mkuu wa kibiashara wa Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako