• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Wakulima wa miwa wagoma Busoga

    (GMT+08:00) 2019-07-03 19:48:55

    Wakulima wa miwa katika eneo la Busoga nchini Uganda wamegoma kupeleka miwa yao viwandani wakilalamikia kupungua kwa bei kutoka shilingi 128,000 hadi 120,000 kwa tani moja.

    Mwenyekiti wa wakulima hao Issa Budhugo, amesema mgomo huo utaendelea hadi pale viwanda vitakapoongeza bei hado shilingi 140,000.

    Lakini naye mwenyekiti wa watengenezaji sukari nchini humo Jim Kabeho, anasema wamepunguza bei baa ya kushuka kwa bei ya sukari sokoni.

    Amesema viwanda vina sukari nyingi ambayo awali ilitarajiwa kuuzwa kwenye masoko ya nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako