• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Nexus Holding ya Saudi Arabia na Akagera Aviation zasaini makubaliano

    (GMT+08:00) 2019-07-03 19:49:13
    Kampuni ya Nexus Holding Group ya Saudi Arabia na Akagera Aviation zimesaini makubaliano ya kutoa mafunzo ya wahadisi na marubani nchini Rwanda.

    Chini ya ushirikiano huo sasa taasisi ya mafunzi ya urubani Akagera imepanda daraja na kuwa na uwezo wa kutoa mafunzo ya hali ya juu.

    Akagera Aviation itakuwa na mgao wa asilimia 40 huku nayo ya Saudi Arabia ikiwa na asilimia 60.

    Akizungumza wakati wa kutiwa saini kwa makubaliano hayo, waziri wa miundo mbinu balozi Claver Gatete, amesema marubani wazawa wa Rwanda ni chini ya asilimia 10 tu lakini kufuatia ushirikiano huo mpya nchi hiyo inatarajia kutoa mafunzo kwa idadi kubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako