• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Tanzania kupiga vita bidhaa gushi

    (GMT+08:00) 2019-07-03 19:49:37
    Makamu wa Rais, wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameonya Tanzania kuwa dampo la bidhaa hafifu huku akisisitiza kuwa serikali haitakubali kuruhusu bidhaa za nje zisizo na ubora kuingia nchini.

    Samia alisema hayo wakati akifungua Maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Maonyesho ya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.

    Ili kuhakikisha mianya inazibwa, aliiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara kudhibiti kuingia kwa bidhaa zisizo na ubora kutoka nje ili kuzipa nafasi bidhaa za ndani.

    Alisema ni vyema ikahakikisha bidhaa zinazotoka nje zinakuwa zenye ubora tu ambazo zina uwezo wa kuleta changamoto kwa bidhaa za ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako