• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Kampuni ya maziwa ya New KCC yapunguza bei ya maziwa kwa Sh5

    (GMT+08:00) 2019-07-04 19:13:06

    Kampuni ya maziwa ya New KCC imepunguza bei ya bidhaa hiyo kwa Sh5 kufuatia ongezeko la maziwa la asilimia 25 kutoka kwa wakulima.

    Bei ya pakiti ya maziwa ya nusu lita sasa itakuwa Sh50 kutoka Sh55.

    Mkurugenzi Mkuu wa New KCC Nixon Sigey anasema kampuni hiyo imeshusha bei kutokana na kuongezeka kwa usambazaji wa maziwa,hivyo basi wanasambaza manufaa hayo kwa wanunuzi ambao wamekuwa wakinunua bidhaa hiyo kwa bei za juu katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

    Alisema bei hizo mpya zilianzishwa tarehe 2 Julai na zinafaa kutekelezwa na wauzaji wa reja reja.

    Sigey alisema ijapokuwa kampuni ya New KCC haijafika katika viwango ilivyokuwa miezi miwili iliyopita,viwango vya maziwa viliyopo vinatosha kubadilisha bei ya bidhaa hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako