• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda-Mashine kutoka China kuagizwa na Kampuni ya Agroplast ili kuzalisha upya bidhaa za plastiki

    (GMT+08:00) 2019-07-04 19:13:25
    Wawekezaji wanaoendesha kampuni ya kutengeza upya mifuko ya plastiki na bidhaa nyingine za plastiki hadi vifaa vingine vinavyotumika katika kilimo na ujenzi,wanatarajia kuanza kutengeza upya kwa kiwango kikubwa chupa za plastiki zinazotumika mara moja,kufuatia marufuku ya chupa hizo nchini Rwanda.

    Léon Nduwayezu, mwenye kampuni ya Agroplast Ltd alikuja na wazo la kutengeza upya bidhaa za plastiki mwaka 2007 wakati ambapo Rwanda ilipiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki.

    Alisema wanatengeza upya zaidi ya tani 1 ya plastiki kila siku.

    Aliongeza kuwa hivi sasa wanashirikiana na Mamlaka ya Mazingira Rwanda kuona ni jinsi gani watazitengeza upya bidhaa za plastiki za matumizi ya mara moja kama vile chupa,mirija na nyenginezo.

    Aidha Nduwayezu alisema wamepata ufumbuzi wa wazo lao na hivi karibuni wataagiza mashine kubwa kutoka China itakayokuwa na uwezo wa kuzalisha upya bidhaa za plastiki na kutengeza vigae na bidhaa nyengine za ujenzi.

    Bunge la Rwanda hivi karibuni liliptisha sheria ya kupiga marufuku utengezaji,uagizaji na uuzaji wa bidhaa z plastiki za matumizi ya mara moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako