• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda-Viwanda vya samaki vyafunguliwa upya kufuatia ongezeko la samaki

    (GMT+08:00) 2019-07-04 19:13:44
    Takriban viwanda vinne vya samaki ikiwa ni pamoja na Marine and Agro, Ngege, Iftra na Gomba Fish vimeanza operesheni kufuatia ongezeko la samaki nchini Uganda.

    Viwanda hivyo vinne,kulingana na Chama cha Wazalishaji na Wauzaji Samaki cha Uganda (UFPEA),vilifungwa yapata miaka mitano iliyopita kutokana na viwango vidogo vya samaki na utendaji mbaya wa sekta hiyo.

    Mwaka 2011,takriba viwanda 10 vya samaki vilifungwa wakati nchi ya Uganda ilipokabiliwa na usambazaji mdogo wa samaki kutokana na mbinu mbovu za uvuvi.

    Hata hivyo akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana,Mwenyekiti wa UFPEA,Bw Sujal Goswami alisema hifadhi ya samaki hivi sasa imeongezeka kutokana na serikali kuingilia kati.

    Kulingana na Benki Kuu ya Uganda,mauzo ya samaki nje ya nchi kwa mwaka 2018 yaliimarika hadi $215m kutoka $124m mwaka 2008.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako