• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya biashara ya China yasisitiza kuwa kama China na Marekani zikifikia makubaliano, ongezeko la ushuru lazima lifutwe

    (GMT+08:00) 2019-07-04 19:44:49

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng hapa Beijing amesema, timu za uchumi na biashara za China na Marekani zinaendelea kuwasiliana. Marekani kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China kwa upande mmoja, ni chanzo cha mikwaruzano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili. Kama pande hizo mbili zikiweza kufikia makubaliano, ushuru ulioongezwa lazima ufutwe.

    Bw. Gao amesisitiza kuwa makubaliano hayo yanatakiwa kuwa na uwiano, usawa na kunufaishana, na ufuatiliaji wa kiini wa China unatakiwa kuridhishwa.

    Ameongeza kuwa China inaitaka Marekani kutimiza ahadi ya kuziruhusu kampuni za Marekani kuuza bidhaa kwa kampuni ya Huawei haraka iwezekanavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako