• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje yasema haipaswi kuamua uhusiano wa China na Marekani kwa upendeleo

    (GMT+08:00) 2019-07-04 19:46:15

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Bw. Geng Shuang amejibu kwa barua wazi yaliyoandikiwa na watu wa sekta mbalimbali wa Marekani kwa rais wa Marekani Donald Trump na bunge la nchi hiyo kwenye gazeti la Washington Post, na kukubali sauti na maoni yenye mantiki na bila upendeleo, na kusisitiza kuwa haipaswi kuamua uhusiano wa sasa wa China na Marekani kwa utata na mikwaruzano.

    Jana wataalamu 95 wa Marekani kutoka sekta za taalama, diplomasia, jeshi na biashara wameandika barua ya pamoja kwa Rais Trump wakisema Marekani ikiichukulia China kama adui, itajidhuru, hali ambayo imeonesha kuwa hakuna Makubaliano ya Marekani yanayounga mkono Marekani kuichukulia China kama adui. Barua hii pia imetoa mapendekezo saba kwa uhusiano wa China na Marekani.

    Bw. Geng ameongeza kuwa China na Marekani si maadui, katika miaka 40 tangu uhusiano wa kibalozi kati ya China na Marekani uanzishwe, uhusiano wa nchi hizo mbili umepata maendeleo ya kihistoria, na kuwaletea faida kubwa kwa watu wa nchi hizo mbili na kuhimiza amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako