• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na mwenyekiti mteule wa Baraza kuu la 74 la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2019-07-04 20:37:01

    Waziri mkuu wa China Bw Li Keqiang leo amekutana na mwenyekiti mteule wa Baraza kuu la 74 la Umoja wa Mataifa Bw. Tijjani Muhammad-Bande mjini Beijing.

    Bw. Li amempongeza Bw. Bande kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza hilo la 74, akisema Umoja wa Mataifa umefanya kazi muhimu katika kulinda amani na usalama wa dunia, kuhimiza maendeleo ya dunia na ushirikiano wa kimataifa. Mwaka kesho itatimia miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, China itaendelea kulinda kithabiti mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, kushikilia kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kulinda usawa na haki ya dunia, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Wakati huo huo, Bw. Li Keqiang leo amekutana na mwenzake wa Bangladesh Bibi Sheikh Hasina Wazed mjini Beijing. Bw. Li amesema China inapenda kudumisha mawasiliano ya ngazi ya juu na Bangladesh, kuimarisha uaminifu wa kimkakati na ushirikiano wa kunufaishana, na kuhimiza uhusiano kati ya nchi mbili upate maendeleo mapya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako