• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: Kombe la dunia daraja la pili (JWRT)-Chipu tayari kuelekea Brazil licha ya ukata

    (GMT+08:00) 2019-07-05 09:52:41
    Timu ya Kenya ya raga ya wanaume ya wachezaji 15 kila upande wasiozidi umri wa miaka 20 almaarufu Chipu jana usiku imeondoka kuelekea Brazil kushiriki mashindano ya raga ya dunia ya daraja ya pili (JWRT).

    Licha ya kuahidiwa usaidizi toka serikalini ilipofuzu michuano hiyo baada ya kuichapa miamba ya Namibia 21-18 jijini Nairobi mnamo April 7, Chipu imekuwa ikikumbwa na ukata.

    Taarifa kutoka Shirikisho la raga nchini Kenya (KRU) kupitia mwenyekiti wake Oduor Gangla zinasema, Chipu inahitaji shilingi 13 milioni za Kenya katika bajeti yake kwa michuano hiyo inayoshirikisha mataifa nane.

    Kundi A linashirikisha mataifa ya Kenya, wenyeji Brazil, Japan na Uruguay. Huku kundi B lina timu za Tonga, Ureno, Canada na Hong Kong. Michuano hiyo itaanza Julai 9 kwa Kenya kuvaana na Uruguay

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako