• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON 2019) Leo mtoto hatumwi dukani, Uganda Cranes uso kwa uso na Simba wa Teranga ya Senegal, Morocco na Benin

    (GMT+08:00) 2019-07-05 09:53:00
    Michuano ya hatua ya 16 bora ya mtoano ya kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) itaanza kupigwa leo mjini Cairo Misri, mchezo unaoangaliwa zaidi ni kati ya wawakilishi wa pekee wa Afrika Mashariki, Uganda Cranes watakapowavaa Simba wa Teranga ya Senegal kwenye mchezo unaotabiriwa kuwa mkali.

    Mchezo mwingine utakuwa baina ya Morocco na Benin, huku kesho zitapigwa mechi kati ya wenyeji Misri na Afrika Kusini nao mchezo unatolewa macho je Afrika Kusini watafanikiwa kuwaangusha Mafarao wa Misri mjini Cairo? Nigeria wao watavaana na Cameroon mjini Alexandria. Julai 7, Madagascar wataumana na DR Congo mjini Alexandria huku Algeria wao watamenyana na Guinea mjini Cairo. Julai 8 zitapigwa mechi mbili kati ya Mali na Ivory Coast mjini Suez na Ghana watakutana na Tunisia mjini Ismailia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako