• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo la kaskazini mwa Afghanistan lashambuliwa kwa mizinga na raia wanne wameuawa

    (GMT+08:00) 2019-07-05 17:29:08

    Polisi wa Afghanistan wamesema soko na makazi ya raia yaliyoko mkoani Faryab, kaskazini mwa nchi hiyo yameshambuliwa kwa mizinga leo asubuhi, na kusababisha vifo vya raia wanne na wengine 36 kujeruhiwa.

    Msemaji wa kituo cha polisi cha mkoa wa Faryab Bw. Abdul Karim Yurish amesema wapiganaji wa Kundi la Taliban walirusha makombora mengi. Kabla ya tukio hilo kutokea, vikosi vya usalama vilipambana kwa risasi na wapiganaji wa Kundi la Taliban. Mapambano hayo bado yanaendelea, vikosi vya usalama vinajaribu kuwafukuza waasi hao, ili kuhakikisha amani na utulivu wa eneo hilo. Kundi la Taliban bado halijasema lolote kuhusu tukio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako