• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wauzaji ramani kiholela washukiwa

    (GMT+08:00) 2019-07-05 17:35:08
    Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), imewataka wafanyabiashara wa ramani za majengo nchini kuacha kuuza ramani hizo mara moja kwani zimekuwa ni chanzo kikubwa cha ujenzi holela usiozingatia viwango vya ubora. Bodi hiyo imesema kumekuwa na matatizo ya kuporomoka kwa majengo, nyumba kuwa na nyufa pamoja na ujenzi unaoziba miundombinu mingine.

    Imesema hali hiyo inayotokana na wenye nyumba wengi kutofuata sheria za ujenzi pamoja na viwango vya ubora.

    Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk. Ludigija Bulamile, alisema watu wanaouza ramani hawaangalii wala kupima viwango vya ujenzi unaotakiwa mahali husika.

    Alisema kuna maeneo hayaruhusiwi kujenga nyumba za ghorofa au nyumba kubwa kutokana na ardhi iliyopo, na wakati mwingine ardhi inakuwa na maji, hivyo kuhitaji msingi mkubwa na mchanganyiko wa zege imara. Lakini watu wananunua na kujenga kwenye maeneo hayo bila kuzingatia athari zinazoweza kutokea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako