• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yasema inaongeza usafi wa uranium iliyorutubishwa

    (GMT+08:00) 2019-07-07 16:50:23

    Msemaji wa serikali ya Iran Bw. Ali Rabiee amesema leo Iran inaanza kuongeza usafi wa uranium inayorutubishwa hadi kiwango cha juu kuliko asilimia 3.67, ambayo ni kikomo kilichowekwa na makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015.

    Bw. Rabiee ameongeza kuwa huu ni uamuzi rasmi, na usafi wa kiwango utategemea mahitaji ya nchi hiyo.

    Wakati huohuo ofisa mmoja mwandamizi wa Iran ametangaza kuwa Marekani inaweza kushiriki katika raundi mpya ya mazungumzo ya nyuklia yaliyoyosainiwa na Iran na pande nyingine zilizosaini makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 zinapanga kuanzisha katika siku za baadaye.

    Mwaka mmoja baada ya Marekani kujitoa kwenye makubaliano hayo, Iran ilijitoa kwenye baadhi ya sehemu ya makubaliano hayo Mei 8, na kutishia kuchukua hatua zaidi kama maslahi yake hayataweza kuhakikishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako