• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • COPA AMERICA: Brazil walitia mikononi kombe la Copa America baada ya kulimezea mate kwa miaka 12

    (GMT+08:00) 2019-07-08 14:06:20

    Tukiangazia michuano ya kombe la Copa America jana usiku pia ilikuwa fainali ambapo wamehitimisha kwa Brazil kuishinda Peru kwa 3-1 na kulitia mikononi kombe kwa mara ya kwanza baada ya kulimezea mate kwa miaka 12. Katika kitimtim hicho Gabriel Jesus alishinda goli moja na kusaidia goli jingine kabla ya kutolewa nje kwa kulimwa kadi ya njano mara ya pili katika kipindi cha pili zikiwa zimesalia dakika ishirini kipenga cha mwisho kupulizwa. Hata hivyo penalti ya dakika za mwisho ya Richarlison ikaihakikishia Brazil Ushindi ambao umekuwa faraja kubwa kwa Jesus, ambaye alitoka kiwanjani huku akilia na kupiga teke chupa ya maji kwa hasira. Naye Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina ambaye pia ndiye nahodha wa kikosi hicho, Lionel Messi juzi usiku alirambwa kadi nyekundu ya pili katika maisha yake ya soka tangu mwaka 2005 alipopata kadi nyekundu ya kwanza. Kwenye mchezo huo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya Copa America, Argentina walishinda goli 2-1 dhidi ya Chile na Lionel Messi akagoma kabisa kupanda jukwaani kwenda kuchukua medali za mshindi wa tatu ambayo ni shaba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako