• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AFCON: Madagascar na Algeria zajikatia tiketi ya robo fainali kombe la Mataifa ya Afrika

    (GMT+08:00) 2019-07-08 14:06:40

    Tukitupia macho sasa kombe la Mataifa ya Afrika jana ilichezwa michezo miwili wa kwanza ulikuwa kati ya Madagascar na DR Congo, na wa pili ulikuwa kati ya Algeria na Guinea. Madagascar ilifanikiwa kujikatia tiketi ya kuingia robo fainali baada ya kuigaragaza DR Congo kwa magoli 4-2 katika hatua ya kupigiana mikwaju, baada ya mpira kumalizika wakiwa wametoshana nguvu kwa mabao 2-2. Na kwa upande wa mechi kati ya Algeria dhidi ya Guinea, Riyad Mahrez alishinda goli la aina yake na kuzidi kuwapaisha juu Mbweha hao wa jangwani huku Guinea wakiporomokwa na mabega baada ya kunyeshewa mvua ya magoli 3-0 huko Cairo na kujiwekea nafasi yao katika hatua ya robo ya fainali ya michuano hiyo. Katika robo fainali Algeria itavaana na Mali au Ivory Coast siku ya Alhamis, huku Madagascar ikicheza na Ghana au Tunisia siku hiyohiyo ya Alhamis. Hata hivyo kwenye michuano hii kumeshuhudiwa habari mbaya kwa nchi ya Misri kumfuta kazi kocha wao mkuu Javier Aguirre baada ya wenyeji kupata kichapo cha mbwa walipocheza na Afrika Kusini kwenye hatua ya 16 ya kombe la Mataifa ya Afrika. Mfarao hao walipewa nafasi kubwa kabla ya michuano lakini walirambwa goli 1-0 baada ya Thembinkosi Lorch kuishindia timu yake katika dakika ya 85. Naye rais wa Chama cha Soka cha Misri Hany Abo Rida ameachia ngazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako