• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga vikali Uingereza kuingilia mambo ya Hong Kong

    (GMT+08:00) 2019-07-08 17:00:58

    Balozi wa China nchini Uingereza Bw. Liu Xiaoming amesema China "inapinga vikali" Uingereza kuingilia mambo ya ndani ya Hong Kong na kuwakosoa baadhi ya wanasiasa wa Uingereza kuwa na mawazo ya vita baridi kwenye uhusiano kati ya pande mbili.

    Akiongea kwenye mahojiano na BBC, balozi Liu amesema kuifanyia marekebisho sheria kuhusu wahalifu wanaotoroka ni jambo linaloeleweka, kwa kufanya hivyo serikali ya utawala maalum ya Hongo na mkuu wa mkoa huo Bibi Carrie Lam wana lengo la kuifanya Hong Kong nzuri na salama zaidi, na sio kuwa maficho ya wahalifu.

    Amesema serikali ya China imeiacha serikali ya utawala maalum ya Hong Kong ishughulikie mambo yake, badala yake serikali ya Uingereza inajaribu kuingilia, na kuwaunga mkono waandamanaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako