• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yatoa mwito utatuzi wa amani wa suala la Iran kuongeza usafishaji wa uranium

    (GMT+08:00) 2019-07-08 17:01:19
    Jumuiya ya kimataifa imetoa mwito wa kutafuta suluhu ya amani baada ya Iran kutangaza kuwa inaongeza kiwango cha uranium cha kusafisha zaidi ya ukomo uliowekwa na makubaliano ya kimataifa ya mwaka 2015.

    Msemaji wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran Bw. Behrooz Kamalvandi leo ametangaza kuwa serikali ya Iran imeanza kusafisha Uranium kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 3.67, na kiwango chenyewe kitategemea mahitaji.

    Viongozi wa nchi mbalimbali wameeleza wasiwasi kuhusiana na hatua mpya ya Iran ambayo inakiuka zaidi makubaliano ya nyuklia na kutaka kuwe na njia ya amani ya kutatua suala hilo.

    Rais Donald Trump wa Marekani ameionya Iran iwe makini, na waziri wa mambo wa nje wa Marekani Bw, Mike Pompeo amezitaka nchi nyingine zihimize Iran isisafishe Uranium. Wizara ta mambo ya nje ya Uingereza imesema wakati Uingereza inaendelea kuheshimu makubaliano hayo inaitaka Iran iache kukiuka wajibu wake kwenye makubaliano hayo.

    Wakati huohuo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang amesema China imesikitishwa na hatua ya Iran kuendelea kutofuata ahadi yake juu ya Makubaliano ya Nyuklia na ameongeza kuwa shinikizo la juu linalotolewa na Marekani dhidi ya Iran ni mzizi wa kuibuka kwa mzozo mpya unaotokea kuhusu suala la nyuklia la Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako