• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Dunia yasifu reli ya kasi ya China

    (GMT+08:00) 2019-07-08 20:09:29

    Ripoti ya utafiti ya Benki ya Dunia imesema, uzoefu wa maendeleo ya reli ya kasi ya China ni mfano wa kuigwa kwa nchi mbalimbali duniani.

    Ripoti hiyo imesema, mpango kamili na vigezo sanifu ni sababu muhimu ya mafanikio ya reli ya kasi ya China ambapo vigezo sanifu vimepunguza gharama za ujenzi wa reli hiyo kwa asilimia 33.3 ikilinganishwa na nchi nyingine.

    Mkurugenzi wa idara ya China ya Benki hiyo Bw. Martin Raiser amesema, China imejenga mtandao mkubwa zaidi wa reli duniani ambao umeleta mabadiliko katika mfumo wa maendeleo ya miji, ongezeko la utalii na uchumi wa kikanda. Pia amesema mtandao huo utatoa mchango katika kupunguza hewa chafu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako