• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: PSG kumchukulia hatua kali Neymar kwa kutofika mazoezini bila taarifa

  (GMT+08:00) 2019-07-09 10:44:57

  Klabu ya Paris St-Germain imesema itamchukulia hatua kali mshambuliaji wa Brazil Neymar baada ya kushindwa kufika mazoezini katika siku ya kwanza kabla msimu kuanza. Mshambuliaji huyo ambaye anahusishwa kutaka kurejea tena kwenye klabu yake ya zamani Barcelona, alitakiwa kurejea mazoezini jana Jumatatu. Katika mahojiano na La Parisien, Mkurugenzi wa michezo wa PSG Leonardo amesema Neymar anaweza kuondoka kwenye klabu hiyo, kama kutakuwa na ofa itakayomridhisha kila mmoja. Hata hivyo chombo cha habari cha Brazil kilimnukuu baba yake Neymar, akisema PSG wanafahamu kwamba mchezaji huyo asingefika mazoezini kwa vile alikwenda kushiriki shughuli ya hisani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako