• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Wimbledon yamlima faini Serena Williams kwa kuharibu uwanja wa michezo

    (GMT+08:00) 2019-07-09 10:45:34

    Mcheza tenisi wa Marekani Serena Williams ametozwa faini ya dola za Kimarekani 10,000 kwa kuharibu uwanja wa Wimbledon kwa kutumia raketi yake. Tukio hilo lilitokea wakati akiwa mazoezini kwenye klabu ya All England kabla ya mashindano. Bingwa huyo wa mara saba wa Wimbledon, anacheza michuano yake ya sita mwaka 2019 na jana alimshinda Carla Suarez Navarro na kujijatia tiketi ya kuingia robo fainali. Naye mcheza Tenisi wa Italia Fabio Fognini amepigwa faini ya dola 3,000 za kimarekani baada ya kusema kwamba Wimbledon ipigwe mabomu. Mchezaji huyo mwenye miaka 32 alisema maneno hayo Jumamosi kwa lugha yake ya kitaliano katika mchezo wake wa raundi ya tatu ambapo alishindwa na Tennys Sandgren.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako