• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • HANDIBOLI: Nairobi Water yatetea ufalme wa handiboli ya wanawake

    (GMT+08:00) 2019-07-09 10:45:52

    Nairobi Water imetetea taji la Super Cup katika handiboli ya wanawake baada ya kutoka chini mabao 13-11 na kuizaba Ulinzi (KDF) magoli 26-22 katika fainali iliyopigiwa ugani Kaloleni Nairobi. Nairobi Water ya kocha Jack Herbert, iliendelea kutembeza kichapo dhidi ya wapinzani wao na kuhifadhi ubingwa huo kwa mara ya tano mfululizo. Licha ya kutoka chini kwa mabao 13-11 vipusa hao waliteremsha mechi safi na kuwaelemea mahasimu wao. Brenda Musambi alichangia kwa magoli saba huku Melvin Akinyi na Brenda Ariviza kila mmoja akiifungia mabao matano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako