• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AFCON: Tunisia na Ivory Coast zasonga mbele hatua ya robo fainali

    (GMT+08:00) 2019-07-09 10:46:06

    Katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika jana ilikuwa ni zamu ya Mali dhidi ya Ivory Coast, na Tunisia walikwaana na Ghana. Katika mechi ya Mali dhidi ya Ivory Coast Wilfried Zaha aliipatia timu yake goli la ushindi na kupelekea Ivory Coast kuinyamazisha Mali kwa bao 1-0 na kuingia hatua ya robo fainali. Mshambuliaji huyo wa Crystal Palace, ambaye anahusishwa kuhamia Arsenal katika majira haya ya joto, alipokea pasi safi kutoka kwa Sylvain Gbohouo na kuingiza mpira golini baada ya mlinda mlango wa Mali Djigui Diarra kushindwa kuuzuia. Ivory Coast itavaana na Algeria Alhamis kwenye robo fainali. Nao Tunisia wameishinda Ghana kwa mabao 5-4 katika muda wa kupigiana mikwaju. Baada ya kutoka sare ya 1-1 na kupewa muda wa ziada, Tunisia iliingiza penalti zote tano huku Ghana ikipoteza moja. Ushindi huo ni mzuri kwa Tunisia kwani kama itakumbukwa wamepoteza mara sita mbele ya Ghana katika michuano ya Afrika. Siku ya Alhamisi Tunisia itacheza na Madagascar kwenye robo fainali huko Cairo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako