Kulingana na takwimu zilizopo, waajiri nchini Rwanda wamefurahishwa na nguvukazi ya warwanda kwa asilimia 78, na endapo serikali itatimiza lengo la kutoa mafunzo zaidi, asilimia hii inatarajiwa kufika 85 mwaka wa 2024.
Baadhi ya mikakati iliyowekwa ni kuanzishwa kwa mtaala wenye ushindani mkubwa na kutoa masomo ya kiufundi kwa vijana. Serikali ya Rwanda inapania kutengeneza nafasi za ajira takriban milioni 1.5, kazi ambazo si za shambani ifikapo mwaka wa 2024. Hii ina maana kwamba kila mwaka serikali ya Rwanda itatengeneza nafasi za ajira ambazo ni zaidi ya laki mbili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |