• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wakulima wazindua kiwanda cha kahawa

    (GMT+08:00) 2019-07-09 18:32:47

    Wakulima wa kahawa katika Kaunti ya Tharaka-Nithi sasa wana sababu ya kutabasamu baada ya kuzindua kiwanda cha kusaga kahawa kilichogharimu Sh45 milioni.

    Hii ni baada ya vyama 30 vya ushirika kutoka kaunti hiyo kuungana kisha kukopa Sh40 milioni ambazo walitumia kujenga kiwanda hicho huku serikali ya kaunti nayo ikiwananunulia mashine ya kusaga kahawa kwa kima cha Sh5 milioni.

    Akizungumza wakati wa kuzinduliwa kwa kiwanda hicho, Gavana wa Tharaka-Nithi Muthomi Njuki alisema kwamba lengo lake ni kufufua kilimo cha kahawa ambacho kilikuwa kimeshamiri eneo hilo miaka ya 80.

    Bw Njuki alisema analenga kushirikiana na vyama vya ushirika vya wakulima ili kuongeza uzalishaji na ubora wa kahawa. Kiongozi huyo alisikitika kwamba baadhi ya wakulima waling'oa majani ya kahawa kwenye mashamba yao na kupanda mimea mingine ili kupata fedha baada ya sekta ya kahawa kukumbwa na changamoto kadhaa na kuwasababishia hasara kubwa.

    Mwenyekiti wa vyama vya ushirika vya wakulima Julius Riungu naye aliwashauri wakulima wote kuwasilisha mazao yao ya kahawa katika kiwanda hicho badala ya kuyapeleka katika viwanda vingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako