• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Johnson akataa kuweka wazi kama atajiuzulu endapo atashindwa kutimiza ahadi ya Brexit

    (GMT+08:00) 2019-07-10 08:14:38

    Kiongozi wa chama cha Wahafidhina cha Uingereza Boris Johnson anayeongoza katika mbio za kuwania nafasi ya uwaziri mkuu wa nchi hiyo amerejea tena ahadi yake ya kuitoa Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya Oktoba 31 kama akishinda nafasi hiyo.

    Akizungumza katika mdahalo uliorushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni akiwa na mpinzani wake ambaye ni waziri wa mambo ya nje Jeremy Hunt, Johnson alikataa kusema kama atajiuzulu akishindwa katika nafasi hiyo, na hakutaka kuzungumzia lolote kama atavunja baraza la chini la bunge kama wanasiasa watajaribu kuzuia Brexit bila ya makubaliano yoyote.

    Mdahalo huo umefanyoka wakati upigaji kura ukiendelea kati ya wajumbe 160,000 wa chama cha Wahafidhina kuchagua nani wanataka awe kiongozi wao atakayemrithi waziri mkuu wa sasa wa nchi hiyo, Bi. Theresa May.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako