• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China asema mapambano ya China dhidi ya ugaidi ni sehemu muhimu ya mapambano ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2019-07-10 08:56:49

    Balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu amesema, kampeni ya China ya kupambana na ugaidi na itikadi kali ni sehemu muhimu ya mapambano ya kimataifa dhidi ya ugaidi.

    Balozi Ma amesema hayo katika mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama la Umoja huo kuhusu matishio kwa amani na usalama wa kimataifa, na kuongeza kuwa China pia ni nchi inayoathiriwa na ugaidi. Amesema, ili kukabiliwa na tishio lililopo la ugaidi na itikadi kali, China imechukua hatua thabiti za kupambana na ugaidi na kuondoa itikadi kali kwa kufuata sheria, na imefanikiwa kuzuia matukio ya kigaidi katika sehemu mbalimbali, huku ikihakikisha kwa kiasi kikubwa zaidi haki za msingi za maendeleo na maisha ya watu kutoka makabila yote.

    Wakati huohuo, mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia dawa za kulevya na uhalifu Bw. Yury Fedotov amesisitiza hatua za kipaumbele za kuimarisha juhudi za kukabiliana na tishio hilo kwa dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako