• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Wanariadha wengine wawili wasimamishwa kushiriki riadha kwa kutumia dawa zilizopigwa marufuku

    (GMT+08:00) 2019-07-10 10:59:05

    Bingwa wa mita 10,000 wa michezo ya Jumuiya ya Madola ya Glasgow ya mwaka 2014 na Afrika Joyce Chepkirui na mkimbiaji wa mbio ndefu John Jacob Kibet Kendagor nao wameingia katika orodha ya wanariadha waliosimamishwa kushiriki riadha kwa makosa ya kutumia dawa zilizopigwa marufuku. Chepkirui, ambaye pia alishinda marathoni ya Amsterdam na Honolulu mwaka 2015 licha ya kumaliza wa 10 katika marathoni ya Boston mwaka huohuo, amesimamishwa na Kitengo cha Maadili ya Riadha (AIU) baada ya kuonesha utofauti kwenye alama zake za vipimo au kitaalamu inajulikana kama Pasipoti ya Kibaolojia ya Wanariadha (ABP). Naye Kendagor, aliyemaliza katika nafasi ya sita kwenye Marathon ya Seoul mwaka 2017 kabla ya kuwa wa pili kwenye marathoni za Hamburg na Istanbul mwaka huohuo, amesimamishwa kushiriki riadha kwa kukataa au kushindwa kuwasilisha sampuli zake za vipimo. Kwa mwaka huu idadi ya wanariadha waliosimamishwa au kupigwa marufuku na AIU imefikia 12 kwa makosa ya kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako