• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AFCON: CAF kufanya mkutano wa kupanga ratiba ya kusaka kufuzu kwa Afcon ya Cameroon 2021

    (GMT+08:00) 2019-07-10 10:59:28

    Shirikisho la Soka Afrika (CAF) litafanya mkutano mkuu Alhamis Julai 18 katika Ukumbi wa Aida Ballroom, wa Hoteli ya Marriott, Cairo, Misri na moja ya ajenda ni kupanga ratiba ya kusaka kufuzu kwa Afcon ya Cameroon 2021. Tanzania imepangwa katika chungu cha tatu pamoja na Madagascar, Zimbabwe, Central Africa Republic (CAR), Namibia, Sierra Leone, Msumbiji, Guinea Bissau, Angola, Malawi, Togo, na Sudan. Nchi hizi zimepangwa katika vyungu vitano kwa kuangalia orodha ya viwango vya ubora wa Fifa iliyotoka Juni 14, 2019. Cameroon itakuwa wenyeji fainali hizo za 2021, ikiwa ni mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo 1972 (miaka 49 iliyopita).

    Na kwa upande wa ratiba ya Afcon ya Misri leo Julai 10 kipute cha robo fainali ndio kinaanza ambapo zitashuhudiwa Benin ikishuka kiwanjani dhidi ya Senegal na Nigeria wakivaana na Afrika Kusini. Kesho Julai 11 pia kutakuwa na michezo miwili, Algeria dhidi ya Ivory Coast na Madagascar wakipimana nguvu na Tunisia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako