• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ufaransa kutoa mkopo wa dola milioni 11 kufanikisha miradi ya maendeleo Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-07-10 19:09:34

    Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika la Maendeleo la Ufaransa imeweka ahadi ya kutoa mkopo kiasi cha dola milioni 11 ambazo ni zaidi ya Sh258 bilioni nchini Tanzania kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta maji, umeme na usafirishaji.

    Shirika hilo liliweka ahadi ya kutoa fedha hizo ndani ya miaka mitano, makubaliano yaliyoanza mwaka wa 2017/18 kupitia mradi ya maji Msoma.

    Kwa mujibu wa shirika hilo, sehemu ya fedha hizo pia itatolewa mwaka 2020 kwa ajili ya kuiwezesha Serikali katika utekelezaji wa mradi wa mabasi ya mwendokasi awamu ya tano katika Jiji la Dar es Salaam hivyo itategemea na mipango ya Serikali katika hatua za kuanza mradi huo.

    Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier amesema ahadi ya mkopo huo imeongezeka mara mbili kutoka dola milioni 55 mwaka 2017 hadi dola milioni 110 sawa na zaidi ya Sh258 bilioni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako