• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wanawake wazuru JKUAT kujifunza kuhusu kilimo na ufugaji

    (GMT+08:00) 2019-07-10 19:09:51
    Viongozi wanawake nchini Kenya wanaojiita 'Embrace' wamezuru Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) kwa lengo la kuangazia umuhimu wa kuhifadhi chakula.

    kikundi hicho kimetangaza wazi kuwa kinashabikia vilivyo ajenda nne kuu za serikali na handisheki ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga.

    Walisema lengo lao kuu ni kujionea jinsi JKUAT inavyoendesha maswala yake ya utafiti kuhusu chakula ili nao waweze kupeleka ujumbe huo mashinani na kufanikisha kilimo biashara katika kaunti zao. Wakiwa katika chuo hicho, viongozi hao walijionea mambo mengi yanayostahili kusambazwa vijijini ili mwananchi wa kawaida aweze kujitegemea kwa chakula na wakati huo huo kupata mafanikio kwenye biashara zao za kilimo.

    Baadhi ya mambo waliyojifunza ni pamoja na ufugaji wa samaki, kuku, kilimo cha kuzalisha matunda, mboga na vingine vingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako