• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi wajumbe wa IAEA watoa wito wa kudumisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA

    (GMT+08:00) 2019-07-11 08:54:25

    Bodi ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) jana imefanya mkutano maalumu huko Vienna kutokana na ombi la Marekani, ambapo imekagua na kujadili Iran inavyotekeleza makubaliano ya nyukilia ya JCPOA.

    Mkutano huo umeshirikisha nchi wanachama 35 wa bodi hiyo zikiwemo China, Marekani, Russia, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, na wajumbe kutoka Iran na Umoja wa Ulaya.

    Nchi wajumbe wengi wa bodi hiyo zimetetea kudumisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na wamesikitishwa na hatua ya Marekani kujitoa kwenye makubaliano hayo na kuongeza shinikizo dhidi ya Iran. Nchi hizo pia zimeitaka Iran itekeleze ahadi zake kwa pande zote, na kuunga mkono juhudi za kidiplomasia za pande zinazoshiriki kwenye makubaliano hayo katika kudumisha makubaliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako