• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasema ushirikiano imara kati ya pande tatu ni muhimu kwa operesheni za kulinda amani

    (GMT+08:00) 2019-07-11 09:01:26

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za kulinda amani Bw. Jean-Pierre Lacroix amesema, ushirikiano imara kati ya Baraza la Usalama la Umoja huo, nchi zinazopeleka kikosi au polisi, na Sekritarieti ya Umoja wa Mataifa, ni muhimu kwa kuimarisha operesheni za kulinda amani.

    Bw. Lacroix ameliambia Baraza hilo kuwa, kazi za kawaida za pande hizo tatu zina umuhimu mkubwa katika kuhakikisha mchakato unaendelea. Amesema faida ya ushirikiano kati ya pande hizo tatu sio tu itasaidia usalama wa walinzi wa amani, bali pia itaunga mkono utendaji wa operesheni hizo.

    Mbali na hayo, amewataka wajumbe waliohudhuria mkutano huo kufikiria kuongeza ushirikiano kati ya pande tatu ili kuhakikisha utekelezaji wa operesheni hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako