• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Kamworor ajitosa mbio za mita 10,000 kwenye fainali za Ubingwa wa Huduma za Polisi za Kenya

    (GMT+08:00) 2019-07-11 14:01:35

    Bingwa wa nusu marathoni duniani Geoffrey Kamworor ameamua kujitosa kwenye mbio za mita 10,000 za fainali za ubingwa wa Huduma za Polisi za Taifa zinazoanza leo huko Kasarani, Kenya. Kamworor, ambaye anataka kuiwakilisha Kenya kwenye mbio za mabingwa wa dunia zitakazofanyika Doha mwaka huu, amesema yuko tayari kunyakua taji la Polisi kwa ushindi wake wa mara nne. Hizi zitakuwa ni mbio zake za pili katika msimu huu. Mshindi huyo wa mara mbili wa Nusu marathoni ya dunia na mbio za nyika alisalimisha taji lake la mbio za nyika kwa Waganda Joshua Cheptegei na Jacob Kiplimo, waliochukua medali ya dhahabu na fedha mtawalia Mach 30 nchini Denmark. Hata hivyo Kamworor, mwenye miaka 26, alirejesha tena nguvu zake na kushinda Grand Prix mbio za maili 10 nchini Switzerland May 11.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako