• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Simba Queens kwenda kutafuta uzoefu wa soka Ujerumani

    (GMT+08:00) 2019-07-11 14:01:50

    Timu ya soka ya Wanawake Tanzania Simba Queens itakwea pipa kwenda Ujerumani Jumapili hii na leo Alhamisi watakuwa Ofisi za Wizara ya Michezo kwa ajili ya kukabidhiwa Bendera ya Tanzania. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori amesema, timu yao itakwenda huko kutokana na ushirikiano na Taasisi ya St.Thomas na dhumuni lao ni kuona baadhi ya wachezaji wanapata nafasi ya kwenda kucheza soka ya kulipwa. Magori alisema, wataondoka wachezaji 15, wataalamu wa benchi la ufundi wanne kwa nguvu ya St Thomas na uongozi wa Simba utamgharamia mkuu wa msafara ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Asha Baraka. Timu itakaa Ujerumani kwa muda wa wiki mbili na itacheza mechi tofauti na baadhi ya timu kubwa za kike na zile ambazo zinahitaji wachezaji wenye vipaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako