Haya ni kwa mujibu wa mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo Dkt Alex Mubiru. Alisema kwamba kupandishwa hadhi au daraja kunatokana na uchumi wan chi kufanya vizuri, hususani katika maeneo ya kasi ya ukuaji wa uchumi na kuwa na deni himilivu. Aidha Benki hiyo inajivunia kufanya kazi wka ukaribu na taifa la Tz, ambalo ni miongoni mwa mataifa waasisi wa Benki hiyo. Naye Waziri wa Fedha na Mipango wa Tz Dk. Philip Mango amesema kwamba Benki hiyo ina mtazamo chanya katika maendeleo ya watu na kuwa dira katika mipango ya maendeleo na kuahidi kushirikiana nao vyema katika kukuza uchumi wa Tanzania.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |