• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Marekani kuanzisha tena mazungumzo ya uchumi na biashara kwenye msingi wa usawa na kuheshimiana

    (GMT+08:00) 2019-07-11 19:34:59

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema ujumbe wa uchumi na biashara wa China na Marekani utaanza mazungumzo kwenye msingi wa usawa na kuheshimiana kutokana na matarajio ya marais wa nchi hizo mbili wakati walipokutana huko Osaka.

    Bw. Gao Feng amesema masuala yanayofuatiliwa sana na China yanapaswa kutatuliwa kwa njia mwafaka, akiamini kuwa pande hizo mbili zinaweza kuzingatia ufuatiliaji wa upande mwingine kupitia mazungumzo yenye usawa, na hakika zitatafuta njia ya kutatua masuala hayo, kitendo hicho kinalingana na maslahi ya watu wa nchi hizo mbili na watu wa duniani.

    Habari nyingine zinasema serikali ya Marekani hivi karibuni imeamua kusamehe ushuru wa kiasi cha juu kwa bidhaa 110 za China zinazouzwa nchini Marekani.

    Kuhusu kampuni za China ikiwemo Huawei kuendelea kuwa kwenye orodha ya udhibiti wa uagizaji bidhaa nje ya Marekani, Bw. Gao ameitaka Marekani isimamishe hatua za kutumia nguvu za taifa ikiwemo kutoa shinikizo na kuweka vikwazo dhidi ya kampuni za China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako