• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema suala la Xinjiang halipaswi kuingiliwa na nchi za nje

    (GMT+08:00) 2019-07-11 20:12:46

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang amesema serikali ya China na wananchi wake wana sauti zaidi katika suala la mkoa wa Xinjiang, na nchi yoyote hairuhusiwi kuingilia katika suala hilo.

    Bw. Geng ameyasema hayo baada ya baadhi ya nchi kuliandikia barua Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa UNHRC zikikosoa sera ya China mkoani Xinjiang. Amesema shutuma hizo hazina msingi na zinayafanya masuala ya haki za binadamu kuwa ya kisiasa, na kuingilia kati mambo ya ndani ya China.

    Ameeleza kuwa mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauyghur wa Xinjiang umechukua hatua mbalimbali za kupambana na ugaidi na kuondoa itikadi kali, ikiwemo kuanzisha kituo cha elimu na mafunzo ya ufundi stadi ili kulinda utulivu wake. Katika miaka miwili iliyopita, hakutokea matukio yoyote ya kigaidi, jamii ni tulivu na watu wa makabila tofauti wanaishi maisha mazuri kwa masikilizano.

    Ameongeza kuwa China imewaalika wanadiplomasia, wanahabari, wasomi wa nchi mbalimbali kwenda mkoani Xinjiang na kujionea hali halisi, ambao wamesema wanachoona ni tofauti na jinsi inavyoripotiwa katika vyombo vya habari vya magharibi, na pia imetoa mwaliko kwa makamishna wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwenda kutembelea Xinjiang.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako