• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendeleza juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

    (GMT+08:00) 2019-07-12 09:51:07

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesema, nchi hiyo itaendelea na juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na inapanga kutambulisha hatua zaidi kuimarisha matumizi ya nishati na utoaji wa hewa chafu.

    Akizungumza kwenye mkutano wa kikundi cha viongozi wanaoshughulika na mabadiliko ya hali ya hewa na kupunguza utoaji wa hewa chafu, Li Keqiang amesema China imepata mafanikio dhahiri katika kuboresha mazingira yake ya kiikolojia, na pia utoaji wa hewa chafu umepungua kwa kiasi kikubwa katika miaka iliyopita.

    Hata hivyo waziri mkuu huyo amesema, juhudi zaidi zinatakiwa ili kufanya majadiliano ya pande nyingi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa yaendane na mahitaji ya nchi zinazoendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako