• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA YA DUNIA U-20: Chipu yachambuliwa kama karanga na Uruguay

    (GMT+08:00) 2019-07-12 10:08:29

    Timu ya taifa ya raga ya wachezaji 15 kila upande ya vijana wasiozidi umri wa miaka 20 ya Kenya almaarufu Chipu, ilikaribishwa katika Raga ya Dunia kwa kichapo cha mbwa koko cha alama 63-11 mjini Sao Paulo nchini Brazil, juzi usiku. Alama za Kenya katika mchuano huu wa Kundi A zilipatikana kupitia kwa mguso wa nguvu-mpya Samuel Were naye nahodha msaidizi Dominic Coulson akachangia penalti mbili. Uruguay ilitangaza hali ya hatari mapema ilipoanza kuwa kinara kwa kuwa na alama 7-0 baada ya Sonneveld Malleret kupachika mguso uliondamana na mkwaju kutoka kwa D'Avanzo Ferres katika dakika ya kwanza. Wachezaji wa Chipu walijaribu binafsi kuisumbua Uruguay, lakini walinzi wa Uruguay walikuwa macho kuzuia kufungwa alama zaidi. Katika mahojiano baada ya mechi, Kocha Mkuu wa Kenya, Paul Odera alikiri kuna idara nyingi zinazohitaji kurekebishwa kabla ya mechi ijayo dhidi ya wenyeji Brazil zikiwemo ikabu, mbinu za makabiliano na kujiamini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako